Anipa moyo wake
Anivisha pete yake
Aniandalia karibu naye
Aniona mimi pekee
Sitosheki
Aniambia nenda
Hawezi nipenda
Aniliwaza na hela
Napokea shingo upande
Siondoki
Anipenda Anikera
Aniwacha anipokea
Mbinguni hadi ahera
Kote anipeleka
Sitosheki
Anyamaza Aongea
Anaelewa Anakosea
Twakimbia Twatembea
Twazama Twaelea
Sisaidiki
Yote mazuri, yote mabaya
Nina Juta, Sina haya
Kuwa mtu mzima
Bila shaka ni mlima
lakini
Sitosheki
Siondoki
Sitosheki
Sisaidiki
Terida
No comments:
Post a Comment